WANIAJI WA NYADHIFA TOFAUTI WAPONGEZWA KWA KUWATEUA WAGOMBEA WENZA KIKE.
Mwakilishi wa kike katika bunge la kitaifa kaunti ya elgeiyo marakwet jane kiptoo chabaibai amepongeza hatua ya viongozi wa kiume kuwachagua wanawake kuwa wagombea wenza wao hasa wa ugavana na urais
Kwenye kikao na wanahabari mjini iten, chebaibai amesema hatua hiyo itafanikisha hitaji la usawa wa kijinsia wa thuluthi mbili humu nchini na kusababisha wanawake zaidi kujitosa katika ulingo wa kisiasa