WANGAMATI ATAKIWA KUOMBA MSAMAHA WAKAZI WA BUNGOMA


Gavana wa kaunti ya Bungoma Wyclife Wangamati ametakiwa kuomba msamaha wakazi wa kaunti hiyo kwa matamshi yake kuwa ana damu ya kikundi cha fera.
Kiongozi wa vuguvugu la Bungoma Liberation Zakaria Baraza amesema kuwa wakazi wengi katika kaunti hiyo walidhulumiwa na kikundi hicho ambacho amekitaja kuwa kikundi haramu na kuwa si vyema kwa kiongozi kama yeye kutoa matamshi hayo.
Wakati uo huo Baraza amemsuta gavana wangamati kwa mipango yake ya kuajiri wasimamizi wa mitaa akisema kuwa wapo wafanyikazi wengi ambao walikuwa wakifanya kazi katika serikali yake na hawajalipwa fedha zao.
Ametishia kuongoza maandamano kupinga mipango hiyo huku akitaka fedha ambazo zimetengwa kutumika katika shughuli hiyo kutumika kuwalipa wafanyikazi hao mishahara yao.