WANGAMATI AFIKA MBELE YA SENETI BAADA YA KUSUSIA MIALIKO KADHAA.


Baada ya gavana wa kaunti ya Bungoma Wycliffe Wangamati kukosa kufika mara ya mwisho alipoalikwa na seneti, sasa gavana huyo amefika mbele ya kamati ya seneti kuhusu afya ili kujibu maswali namna amekuwa akitumia fedha ambazo zilitengewa serikali ya kaunti hiyo ili kupambana na janga la korona.
Gavana Wangamati hata hivyo amejitetea kuhusia na hutua ya fedha kupotea zilipokuwa zikitumwa kwenye akaunti za benki za zahanati za Bungoma ili kusaidia kupiga jeki vita dhidi ya virusi vya corona.
Kulingana na Wangamati fedha hizo zilipotea njia kutokana na maafisa husika kwenye serikali ya kaunti hiyo kupeana habari ambazo si sahihi kuhusu akaunti za benki ambako fedha zilistahili kutumwa.
Kulingana na mkaguzi mkuu wa serikali, seriikali ya kaunti ya Bungoma ilitumia pesa za corona bila mpango maalum japo gavana Wangamati amejitetea kwamba mpango ulikuwepo japo walifeli kuwasilisha mapema kwa mkaguzi wa hesabu za serikali.