WANDANI WA RUTO WAKASHIFU KURUGWA NEMBO YA UDA CHEPARERIA.

NA BENSON ASWANI
Viongozi mbali mbali wandani wa naibu rais William Ruto katika kaunti hii ya Pokot magharibi wameendelea kukashifu hatua ya kuondolewa nembo za chama cha UDA za wilbarow zilizokuwa zimetundikwa eneo la Chepareria kwa maandalizi ya ziara ya naibu rais kaunti hii.
Wa hivi punde kukashifu tukio hilo ni mbunge wa kapenguria Samwel Moroto ambaye amedai kuwepo baadhi ya viongozi wa kisiasa katika kaunti hii ya pokot magharibi ambao wanawachochea vijana kuvuruga mipango ya wapinzani wao.
Wakati uo huo Moroto ameilaumu idara ya polisi katika kaunti hii kwa kusalia kimya licha ya kuwa wapo baadhi ya wakazi walioathirika kutokana na tukio hilo la wiki jana, akiwataka polisi kutekeleza majukumu yao ya kulinda usalama jinsi inavyopasa.