WANDANI WA RUTO WAENDELEA KUTETEA SERA ZAKE POKO MAGHARIBI.


Wandani wa naibu rais William Ruto katika kaunti hii ya Pokot magharibi wameendelea kutetea sera za Ruto kuelekea katika uchaguzi mkuu wa mwaka ujao.
Wakizungumza katika mahojiano na kituo hiki, vijana katika chama cha UDA kaunti hii wakiongozwa na Emmanuel Kones wamepuuzilia mbali kauli za wapinzani wa Ruto kuwa anatumia sera ya wheelbarrow kwa kuwa hana la kuwapa vijana wa taifa hili.
Wamesema kuwa Wheelbarrow inatumika tu kama nembo ya chama kuashiria hali ya mwananchi wa chini.
Wakati uo huo vijana hao wamepuuzilia mbali mikutano ya baadhi ya wagombea urais na muungano wa wafanyibiashara wa mlima Kenya Mt Kenya foundation MKF wakisema kuwa mwananchi wa kawaida ndiye aliye na uamuzi kamili wa atakayeongoza taifa hili.