WANDANI WA RUTO WAENDELEA KUPIGIA DEBE AJENDA YAKE YA MAENDELEO.

Na Benson Aswani
Wandani wa naibu rais William Ruto katika kaunti hii ya Pokot magharibi wameendelea kupigia debe mfumo wake wa kuimarisha uchumi Bottom up economic model.
Wakiongozwa na mwakilishi wadi ya Lelan Johnson Lokato, viongozi hao wamesema kuwa wakazi wengi katika kaunti hii wamesalia bila ajira licha ya kukamilisha masomo ya vyuo vikuu na kuwa mfumo wa kiuchumi wa naibu rais ndio utakaoangazia tatizo hilo katika kaunti hii na taifa kwa jumla.
Wakati uo huo Lokato ametoa wito kwa machifu maeneo mbali mbali ya kaunti hii kurahisisha shughuli ya utoaji wa vitambulisho kwa vijana ili kuwapa fursa ya kujisajili kuwa wapiga kura na kushiriki katika uchaguzi mkuu ujao kwani wengi wao hawajajisajili kutokana na ukosefu wa vitambulisho.