WANAWAKE KAUNTI YA POKOT MAGHARIBI WAMETAKA KUHUSISHWA KATIKA SHUGHULI ZOTE AMBAZO WANAUMME WANAFANYA


Wanawake kaunti ya pokot magharibi wanaomba kuhusishwa katika shughuli ambayo inaibuka katika kaunti ya pokot magharibi hii ni baada ya kuonekana kuwa wanawake wengi hawapewi nafasi ya kuongoza katika jamii kutokana na itikadi za jamii ya pokot.
Siku ya kimataifa ya wanawake ni siku inayonuia kusisitiza usawa wa jinsia, ni siku ya kusheherekea hatua ambayo wanawake wameafikia katika jamii katika sekta za siasa, uchumi , elimu na maswala mengine nyeti
Kaunti ya pokot magharibi ni miongoni mwa kaunti ambazo bado zinakumbwa na tatizo la taasubi za kiume, hali inayowapa wanawake changamoto katika kupenyeza kimaisha
Haya ni baadhi ya malamishi ya wanawake wanaoishi kaunti hii
Ikumbukwe, serikali katika kutetea haki za wanawake ilitenga fedha kwa miradi ya wanawake kama uwezo fund kwa kusudi la kuwafikia wanawake zaidi ya milioni hamsini nchini kenya
wanawake wa kaunti ya pokot magharibi wamefaidika kivipi na mradi huo