WANAUME AMBAO WANADAIWA KUWABAKA NA KUWAPACHIKA MIMBA WANAFUNZI ELFU 10 KWENYE KAUNTI YA TRANS NZOIA KUSAKWA


Kamanda wa polisi kwenye kaunti ya Trans Nzoia Fredrick Ochieng’ ameanzisha oparesheni ya kuwakamata wanaume ambao wanadaiwa kuwabaka na kuwapachika mimba wanafunzi elfu 10 kwenye kaunti hiyo.
Hii inafuatia agizo alilotoa waziri wa usalama wa ndani Dkt Fred Matiang’i.
Ochieng amesema kuwa anashirikiana na machifu na idara ya watoto kuwatambua washukiwa.
Akizungumza na wanahabari afisini mwake Ochieng amesem akuwa watakaopatikana watawajibishwa kisheria.
Kadhalika Ochieng’ amewaonya wazazi ambao wanashirikiana na washukiwa kusuluhisha kesi hizo nyumbani bila kuwahusisha polisi akisema kuwa pia watawajibishwa.

[wp_radio_player]