WANASIASA WATAKIWA KUJITENGA NA MASWALA YA HOSPITALI YA KACHELIBA.


Uongozi wa hospitali ya kacheliba kaunti hii ya pokot magharibi umekanusha vikali madai ya kushirikiana na baadhi ya maduka ya kuuza dawa mjini kacheliba kwa lengo la kujinufaisha kifedha.
Kulingana na msimamizi mkuu wa hospitali hiyo solomon tukei, ni kwa uchache sana ambapo madaktari wa hospitali hiyo wamewahi kumtuma mgonjwa kutafuta dawa katika maduka ya kuuza dawa hizo, na kuwa watafanya hivyo iwapo dawa hiyo haitapatikana katika hospitali ya kacheliba.
Aidha tukei amesema hamna duka lolote maalum la kuuza dawa ambalo madaktari wa hospitali hiyo wanawatuma wagonjwa kununua, ila duka lolote ambalo wana uhakika kuwa dawa hizo zitapatikana, na ni kwa uchache sana maana hospitali hiyo ina dawa za kutosha kuwahudumia wagonjwa.
Kwa upande wake muuguzi mkuu wa hospitali hiyo luke kanyang’areng ametoa wito wa kutoingizwa siasa katika maswala ya hospitali hiyo kwa manufaa ya watu binafsi.