WANASIASA WATAKIWA KUHUBIRI AMANI TRANS NZOIA.

Wito umetolewa kwa wanasiasa nchini kuhubiri na kukumbatia amani na utangamano wakati wanapofanya siasa zao za uchaguzi mkuu wa Agosti 9.
Akihutubu wakati wa fainali ya kombe la Pukose iliyoandaliwa katika shule ya msingi ya Endebess kaunti ya Trans nzoia mbunge wa eneo hilo Dkt Robert Pukose amesema ipo haja ya wanasiasa kuheshimiana na kufanya siasa za amani kwa kuuza sera zao na sio kutupa cheche za maneno ambayo huenda yakagawanya taifa hili.
Wakati huo huo Dkt Pukose ameezelea kwamba kwa muda wa miaka 10 ambayo amehudumu kama mbunge wa eneo hilo ameimarisha miundo msingi katika sekta ya Elimu kwa kujenga zaidi ya shule 25 za msingi na shule 15 za upili.