WANASIASA WATAKIWA KUCHUNGA MATAMSHI YAO.


Wito umetolewa kwa wanasiasa nchini kuwa waangalifu na matamshi wanaotoa kwenye kampeni zao za kisiasa wakati huu ambapo wanatafuta uungwaji mkono kwenye nyadhifa mbalimbali za uchaguzi wa Agosti 9.
Akihutubu katika wadi ya Chepsiro Kiptoror mwakilishi wadi eneo hilo Kipchumba Birir amekosoa baadhi ya wanasiasa wanaotoa matamushi ambayo huenda yakagawanya taifa kwa misingi ya vyama au kikabila akisema jambo hilo linafaa kushutumiwa vikali bila ya mapendeleo kwani linazua uhasama miongoni mwa wafuasi pinzani.
Wakati huo huo Birir ametoa wito kwa vijana kutokubali kutumika vibaya na wanasiasa kuzua rabsha kwenye mikutano ya kisaisa na badala yake kusikiza kila kiongozi na kufanya uamuzi wa burasa wakati wa uchaguzi, akisisitiza haja ya kudumishwa kwa amani wakati huu wa kampeni.