WANASIASA WAONYWA DHIDI YA SEMI ZA CHUKI TRANS NZOIA.
Mikakati mwafaka imewekwa kuhakikisha kuwa amani inadumishwa wakati wa uchaguzi mkuu wa mwezi agosti mwaka huu.
Haya ni kulingana na kamshina wa kaunti ya Trans nzoia Sam Ojwang ambaye amesema kuwa serikali iko macho na kamwe haitoyasaza makundi ya watu na viongozi ambao wanatoa kauli za chuki kwa lengo la kuvuruga amani ya nchi.
Ojwang amewataka wanasiasa ambao wanaendeleza kampeni za kutafuta uungwaji mkono kwa wakenya kuhubiri amani na umoja wa wakenya ili kuhakikisha kuwa taifa linasalia pamoja hata baada ya uchaguzi mkuu ujao.