WANASIASA WAONYWA DHIDI YA KUWATISHIA WALIMU POKOT MAGHARIBI.


Katibu mkuu wa chama cha walimu nchini Knut tawi la Pokot magharibi Martine Sembelo ameonya vikali dhidi ya kutishiwa walimu kwa lengo la kuwataka kuunga mkono wanasiasa fulani katika uchaguzi mkuu wa mwezi agosti mwaka huu akitaka walimu kupewa fursa ya kuwaunga mkono wanasiasa wanaowapendelea.
Akizungumza afisini mwake Sembeleo amedai baadhi ya walimu kaunti hii wamekuwa wakipokea vitisho kutoka kwa wanasiasa kwa kudinda kuwaunga mkono, akisema kama viongozi wa walimu kaunti hii hawatakubali hulka hiyo kuendelea kushuhudiwa.
Wakati uo huo Sembelo ameitaka serikali kuleta chakula cha msaada katika kaunti hii ya Pokot magharibi ili kuwawezesha wanafunzi kuhudhuria masomo bila tatizo.
Aidha amewaonya baadhi ya maafisa na walimu kwa jumla katika kaunti hii ya Pokot magharibi dhidi ya kuuza chakula cha wanafunzi akisema hatua kali zitachukuliwa dhidi ya yeyote atakayehusika uovu huo.