WANASIASA TRANS NZOIA WAHIMIZWA KUHUBIRI AMANI KATIKA KAMPENI ZAO.


Wazee kutoka jamii ya luhya katika kaunti ya Trans nzoia wameomba amani kabla wakati na hata baada ya uchaguzi mkuu ujao akiwataka viongozi ambao wanawania viti mbalimbali kuhubiri amani wakati wa kampeini.
Wakiongozwa na mzee abdi wanyama kutoka eneobunge la cheranganyi wameomba viongozi kushirikiana na wazee na kuendeleza kampeini za amani wakati huu ambao taifa linajiadaa kuelekea uchaguzi mkuu wa agosti tisa.
Wamewaomba wananchi kuwachagua viongozi watakaowajibikia changamoto zao bila ya kuwabagua.