WANASIASA POKOT MAGHARIBI WATAKIWA KUSHIRIKIANA KUFANIKISHA MAENDELEO.


Aliyekuwa mwakilishi wadi maalum Lucy Lotee ameshutumu pakubwa malumbano ambayo yanashuhudiwa miongoni mwa wabunge katika kaunti hii kuhusiana na miradi mbali mbali ikiwemo ujenzi wa barabara.
Akizungumza na kituo hiki bi Lotee amewataka viongozi hao kukaa chini na kuelewana jinsi ambavyo miradi hiyo itatekelezwa kwa manufaa ya mkazi wa kaunti hii badala ya kulumbana kila mara huku akikosoa kile ametaja kuwa kujipiga kifua baadhi ya wabunge kuhusu ujenzi wa barabara kaunti hii.
Wakati uo huo Lotee amedai kuwa baadhi ya viongozi wanatumia mbinu hizo kuficha kile amedai ufisadi ambao unaendelezwa nao kupitia miradi ya ujenzi wa barabara.