WANAOWABAKA WATOTO KUTOPEWA MSAMAHA WA RAIS

Aliyekuwa mwakilishi wadi mteule eneo la Endebes kaunti ya Trans nzoia Benedine Omondi anapendekeza watu wanaopatikana na makosa ya kuwabaka watoto wachanga kutopokea msamaha wa rais.

Omondi amesema washukiwa wa visa hivyo wanastahili kutumikia kifungo cha maisha kwa uovu ambao wamewatendea watoto.

Akizungumza katika hafla moja eneo hilo Omondi aidha ametaka wanaohusishwa na mauaji kutoachiliwa katika hali yoyote bali wasalie korokoroni ili kukabili uovu huo miongoni mwa wanajamii.