WANAOPACHIKA MIMBA WANAFUNZI KIPKOMO WAONYWA.

Onyo kali imetolewa kwa watu wenye hulka ya kuwapachika mimba wanafunzi kuwa vitengfo vya usalama viko macho na atakayepatikana hatia ya kutekeleza uovu huo atakabiliwa vikali kulingana na sheria.
Mkurugenzi wa elimu eneo la Kipkomo kaunti hii ya pokot magharibi Evans Onyancha amesema kuwa visa hivi vimerejesha nyuma pakubwa juhudi za kuhakikisha elimu ya mtoto wa kike katika kaunti hii ya Pokot magharibi inaafikiwa kikamilifu.
Amesema kuwa watashirikiana na idara ya usalama kuhakikisha visa hivi vinakabiliwa na kuhakikisba mtoto wa kike anaafikia ndoto yake maishani.
Wakati uo huo Onyancha amesemka kuwa idara ya elimu eneo hilo imeweka mikakati ya kupunguza visa hivyo eneo la Kipkomo ikiwemo kuanzisha kampeni ya kuhamasisha watoto wa kike dhidi ya visa hivi kwa kuwatumia watu hasa wa jinsia ya kike ambao ni kielelezo kwa jamii.

[wp_radio_player]