WANAOENDESHA KAMPENI ZA USIKU WAONYWA BARINGO.
Idara ya usalama kwenye kaunti ndogo ya Eldama ravine kaunti ya baringo imewaonya viongozi wanaowania nyadhifa za kisiasa kwenye uchaguzi mkuu wa agosti 9 dhidi ya kuandaa mikutano nyakati za usiku.
Naibu kamishna eneo hilo omar ali amesema kwamba ni marufuku kwa kiongozi yeyote kandaa mkutano wa kisiasa wakati wa usiku katika kipindi hiki cha kampeini za kuelekea uchaguzi mkuu ujao.
Akiongea katika eneo la koibatek ali amesema kwa wakati mwingine mikutano inayoandaliwa nyakati za usiku ndio hutumika kueneza matamshi ya chuki au uchochezi.
Ali ameonya kwamba watakaokiuka marufuku hayo watachukuliwa hatua za kisheria.