WANANCHI WAVAMIA BOMA LA KASISI MOI’S BRIDGE KAUNTI YA KAKAMEGA


Wananchi waliokuwa na hamaki walivamia boma la kasisi mmoja aliyedaiwa kuwafungia ndani ya nyumba watoto watatu wa kike wa kati ya miaka sita na tisa mtawalia akiwemo mmoja mlemavu kwa madai ya kuwaweka kwenye maombi katikakijiji cha Moi’s Brigde eneo bunge la Likuyani kaunti ya Kakamega.
Wakazi wakiongozwa na Elimina Mmbone walifika bomani mwa kasisi huyo na kulazimika kuuvunja mlango, na kuwapata watoto wameachwa ndani ya nyumba ya kasisi bila ya chakula wa maji.
Wanasema mmoja wa wahusika ambaye ni wa miaka tisa na anayeishi na ulemavu, aligongwa na gari na badala ya wazazi wake kumpeleka hospitalini, waliamua kumpeleka kwa kasisi huyo ambaye anadaiwa kuwafungia ndani ya nyumba anapoondoka na mkewe mapema asubuhi na kisha kurejea masaa ya jioni.
Wenyeji wanataka idara ya polisi kumtia mbaroni mshukiwa pamoja na wazazi wa watoto husika kwa kuwaacha wanao kiholela ikizingatiwa ni watoto wa kike.