WANANCHI WAHITAJIKA KUTOA USHIRIKIANO ZAIDI KATIKA VITA DHIDI YA DHULUMA KWA WATOTO.


Shirika la Topoyo kwa ushirikiano na lile la DSW linalokabiliana na dhuluma dhidi ya watoto linaendeleza uhamasisho kwa jamii kuhusu umuhimu wa kuripoti visa vya dhuluma hizi punde wanapovishuhudia.
Wakizungumza mjini Kacheliba kaunti hii ya Pokot magharibi, maafisa wa shirika hilo wakiongozwa na katibu mkuu Joseph Sarich wamesema kuwa swala la unyanyapaa miongoni mwa waathiriwa wa visa hivyo limesalia changamoto kuu katika vita hivyo.
Maafisa hao wametoa wito kwa jamii kushirikiana na shirika hilo kwa kuripoti visa hivi ikiwemo ndoa za mapema pamoja na ukeketaji ili kumpa nafasi mtoto wa kike kupata elimu na kuafikia ndoto zake maishani.
Wakati uo huo shirika hilo limewahimiza wadau katika idara ya usalama ikiwemo machifu na manaibu wao kuwa msitari wa mbele katika vita dhidi ya visa hivi.