WANAMME WAWILI WAHUKUMIWA KIUFUNGU CHA MIAKA 120 NA 80 MTAWALIA NA MAHAKAMA YA KITALE


Mahakama ya Kitale imewahukumu wanamme wawili kifungu cha miaka 120 na miaka 80 mtawalia gerezani baada ya kushtakiwa kwa wizi wa kimabavu.
Mwanamme mmoja ambaye ametambuliwa kama Walter Mong’are amehukumiwa miaka 120 baada ya kudaiwa kutekeleza uhalifu huo katika miji ya Kitale na Nyamira huku mwenzake Christopher Momanyi naye akihukumiwa kwa kushirikiana na Mong’are katika wizi uliotekelezwa mjini Kitale.
Upande wa mashtaka hata hivyo ulijuzwa kwamba kwenye kisa hicho cha Kitale mtu mmoja aliuawa baada ya kupigwa risasi.