WANAHARAKATI WATAKA SHERIA DHIDI YA MIMBA ZA MAPEMA KUFANYIWA MAREKEBISHO.
NA BENSON ASWANI
Mmoja wa watetezi wa haki za watoto katika kaunti ya Baringo Nyambura Maing’una ameelezea haja ya kutathminiwa upya sheria inayotoa adhabu kwa mtoto mvulana anayempachika mimba msichana mwenye umri wa chini ya miaka kumi na minane.
Kulingana na nyambura ni kwamba sheria za sasa zinamwadhibu mtoto mvulana huku msichana akisazwa licha ya kwamba huwenda walikubailiana kushiriki tendo la ndoa.
Nyambura anasema kuwa mtoto mvulana hastahili kuadhibiwa mahakamani kutokana na kile ametaja kama kosa lililotokana na maelewano baina yake na mwenzake msichana.
Aidha nyambura amewahimiza wazazi kuwa karibu na wanao na kuwazungumzia wazi wazi kuhusu athari za kushiriki ngono wakiwa bado wachanga.