WANAHARAKATI WA HAKI ZA BINADAM WALALAMIKIA GHARAMA YA MAISHA NCHINI.
Wanaharakati wa haki za binadam nchini wameshutumu hatua ya kuendelea kuongezwa bei za mafuta nchini hali ambayo imepelekea kupanda gharama ya maisha wakenya wengi wakishindwa kukidhi mahitaji ya kimsingi kukiwemo kununua chakula matibabu na kuwalipia wanao karo.
Wakiongozwa na Richard Masanja, wanaharakati hao katika kaunti ya Trans nzoia wamesema hali imekuwa hata mbaya zaidi kutokana na kuongezeka kwa bei hiyo ya mafuta.
Aidha Masanja amesema kuwa visa vya uhalifu vimeanza kushuhudiwa hasa wizi akiomba serikali kuweka mikakati ya kuhakikisha bei ya mafuta inapungua.