WANAHARAKATI POKOT MAGHARIBI WAPINGA MAFUNZO KWA WALIMU KUHUSU CORONA.

Na Benson Aswani
Shughuli ya kuwafunza baadhi ya walimu kutoka shule mbali mbali kuhusu jinsi ya kukabiliana na visa vya maambukizi ya corona shuleni iwapo vitaripotiwa, inayoongozwa na shirika la CY Kenya, imakosolewa vikali na baadhi ya wanaharakati katika kaunti hii ya Pokot magharibi.
Wakiongozwa na Abraham Kibet wanaharakati hao wamekosoa jinsi shughuli hiyo inavyoendeshwa hasa ikizingatiwa kila shule inapasa kulipia shilingi alfu 2 kwa kila mwalimu anayepokea mafunzo hayo licha ya kutolewa fedha za kukabili janga la corona huku wakitaka walimu kususia shughuli hiyo.
Kibet ameshutumu tume ya huduma kwa walimu TSC kwa kuagiza kuendeshwa shughuli hiyo akidai kuwa walimu wametishiwa dhidi ya kuisusia, akitaka tume ya maadili na kukabili ufisadi EACC kuingilia kati na kuchunguza matumizi ya fedha zilizotolewa kukabili janga la corona.