WANAHARAKATI BUNGOMA WAAHIDI KUWALIPIA DHAMANA WAFUNGWA


Wanaharakati wa vuguvugu la Bungoma Liberation katika kaunti ya Bungoma wameahidiu kushirikiana na idara ya magereza katika kaunti hiyo kuwalipia dhamana wafungwa ambao wanadaiwa kiwango kisichozidi alfu 10 kila mmoja.
Akitoa ahadi hiyo msemaji wa vuguvugu hilo Isaiah Sakonyi amesema kuwa wapo wafungwa wengi katika magereza ya kaunti hiyo waliokamatwa na wanazuiliwa hali hawana uhatarai wowote kwa jamii kaunti hiyo.
Sakonyi ameyasema hayo baada ya kumlipia dhamana mfungwa mmoja aliyekamatwa kimakosa mjini Chwele kaunti ya Bungoma zaidi ya miezi miwili iliyopita kwa kudhaniwa kuwa mgemaji pombe haramu.
Ameahidi kuwa vuguvugu hilo litamsaidia mwathiriwa kujikimu kiuchumi.