WANAHABARI WAZUILIWA KUINGIA KWENYE MASHULE POKOT MAGHARIBI


Huku leo ikiwa siku ya tatu Wanafunzi wakirejea shuleni kote nchini, hali katika kaunti ya Pokot Magharibi haijabainika wazi baada ya Wanahabari kuzuiliwa kuzuru mashule na kutathmini hali.
Hata hivyo Kalya radio imebaini kwamba wizara ya elimu kaunti ya Pokot Magharibi ilitoa agizo kwa Wakuu wa shule zote ikiwemo za msingi na pia Binafsi kutowaruhusu Waandishi Wahabari kuingia shuleni kutathmini hali ya utayarifu wa shule katika kuzingatia masharti ya wizara ya afya kukabili msambao wa covid 19.
Haya Yanajiri huku kaunti hii ikikisiwa kurekodi viwango vya juu vya mimba za mapema miongoni mwa watoto wasichana, ukeketaji na ndoa za mapema hasa masimu ambapo wanafunzi walisalia nyumbani kwa likizo ndefu ya kanga la corona.
Agizo hilo limedhihibitishwa na Mkurugenzi wa elimu katika kaunti ya Pokot Magharibi Jacob Onyego ambaye amesema alitoa agizo kwa walimu wakuu katika Kaunti hii kutowaruhusu wanahabari kuingia kwenye shule zote kwenye kaunti hii baada yake pia kupewa agizo na wakubwa wake swala ambalo ni la kusikitisha mno.
Kalya radio imebaini kwamba kuzuiliwa kwa wanahabari ni kwa sababu ya Changamoto nyingi ambazo shule nyingi katika kaunti hii zinashuhudia ikiwemo ukosefu wa maji, uhaba wa madarasa na madawati ya kutosha ikizingatiwa kwamba serikali kuu haijatimiza ahadi ya kusambaza madawati kwa asilimia kubwa ya shule katika kaunti hiyo.
Swali ni je iwapo wanafunzi zaidi ya mia nane na zaidi kufikia juni mwaka jana kaunty ya pokot magharibi walikuwa wameripotiwa kupachikwa mimba tangu shule zilipofungwa ghafla mwezi machi mwaka uliopita baada ya kuzuka kwa janga la korona kwa sasa hali katika shule za kaunty ya Pokot iko vipi hadi kufikia leo.ni baadhi tu ya mambo ambayo wizara ya elimu inajaribu kuzuia wanahabari kufichua.
Ikumbukwe kwamba vyombo vya habari tangu jadi vimekuwa msatari wa mbele kuangazia hali katika shule mbalimbali hasa mikakati iliyowekwa na serkali ilikuzuia maambukizi ya virusi vya corona huku ikibainika kwamba shule nyingi hazina mazingira ya kuridhisha kaunty ya pokot magharibi kwa wanafunzi kusomea.