WANAFUNZI WENGI KAUNTI YA POKOT MAGHARIBI WAMENGAA KATIKA MTIHANI WA KITAIFA WA KCPE

Shule ya msingi ya Town View katika kaunti hii ya Pokot magharibi ni miongoni mwa zilizotia fora kwenye mtihani wa kitaifa wa darasa la nane KCPE mwaka huu ambao umetangazwa jana na waziri wa elimu Prof. George Magoha.
Kulingana na matokeo ambayo tumeyapokea kufikia sasa, mwanafunzi bora katika Onyango Michael Oluoch amepata alama 417, Ngolepus Marion Chelimo akiwa wa pili bora kwa alama 415 huku Komongiro Jerome akifunga tatu bora katika shule hiyo kwa alama 414.
Rebecca Lotuliatum ni mkurugenzi wa shule hiyo

Aidha wanafunzi waliofanya vyema wameelezea kuridhishwa na matokeo huku wazazi wakisifia juhudi za walimu wa shule hiyo kwa juhudi ambazo walitia katika kuhakikisha shule hiyo infanya vyema.

Katika shule ya msingi ya st Marys mwanafunzi bora ni Trevour Limo ambaye alipata alama 415 akifuatwa na Gracious Apiaro kwa alama 413.

Kulingana na matokeo hayo zaidi ya wanafunzi kumi katika shule hiyo wamepata zaidi ya alama 400 katika mtihani huo.
Kulingana na matokeo ambayo yametufikia kufikia sasa shule ya hiyo ya st Marys ndiyo inayoongoza kaunti hii kwa kusajili jumla ya alama 382, ikifuatwa na town view ambayo imesajili alama 375 huku makutano central ikisajili alama 318.

Gilbert Situma ni mwalimu mkuu wa shule ya msingi ya st marys.

Aidha mwanafunzi wa kwanza katika shule ya msingi ya Sebit amepata alama 382 huku mwanafunzi wa kwanza katika shule ya msingi ya Orolwo akipata alama 325.