WANAFUNZI WALIOACHIA DARASA LA NANE KUENDELEA NA MASOMO YAO KATIKA CHUO CHA KIUFUNDI CHA KITALAKAPEL


Chuo cha kiufundi cha Kitalakapel katika kaunti hii ya Pokot Magharibi kimeanzisha kozi kwa ajili ya wanafunzi ambao waliachia masomo yao katika darasa la nane.
Akizungumza siku moja tu baada ya kuzinduliwa rasmi chuo hicho na naibu rais William Ruto, mkuu wa chuo hicho John Kibowen amesema hatua hiyo imechochewa na hali kuwa wapo wanafunzi wengi miongoni mwa jamii ambao hawakuweza kuendelea na masomo baada ya darasa la nane na sasa wanatoa fursa hiyo kwa wanafunzi hao.
Aidha Kibowen amesema kuwa chuo hicho ndicho cha kipekee ambacho kinashughulikia mswala ya kilimo kanda nzima ya kaskazini mwa bonde la ufa ikiwa kutengeneza bidhaa zinazotokana na maziwa, matunda pamoja na nyama.
Kwa upande wake mwakilishi wadi ya Riwo David Alukulem ametoa wito kwa naibu rais William Ruto kuendelea kushika mkono chuo hicho ikiwemo kujenga vyumba vya kulala na kuhakikisha kinaunganishiwa umeme kwani kimekuwa cha manufaa zaidi kwa wakazi wa eneo hilo.