WANAFUNZI WAHIMIZWA KUDUMISHA NIDHAMU WANAPOKUWA SHULENI
Na Benson Aswani
Wanafunzi wanapasa kupewa fursa ya kudhihirisha uwezo wao wa uongozi kupitia fursa mbali mbali za uongozi shuleni.
Akizungumza wakati wa shughuli ya uchaguzi wa viongozi mbali mbali wa wanafunzi ambao unaandaliwa katika shule ya upili ya Chewoyet, mwalimu mkuu wa shule hiyo Samwel Kiminisi amesema kuwa uongozi bora nchini huanzia shuleni.
Kiminisi ametoa wito kwa walimu wakuu katika shule mbali mbali kaunti hii ya Pokot magharibi kutoa fursa kwa wanafunzi kuandaa chaguzi hizo kwa kuwapa mwelekeo unaostahili kwani ni kupitia hali hiyo ambapo taifa litapata viongozi waadilifu na wenye tajriba ya kutosha siku za usoni.
Kiminisi ametumia fursa hiyo pia kuwashauri vijana kuwa waangalifu na kutokubali kutumiwa na wanasiasa visivyo kwa manufaa yao ya kisiasa na badala yake kutumia fursa hiyo kuwapiga msasa wanasiasa wote ili kufanya uamuzi wa busara katika uchaguzi mkuu wa mwaka ujao.