WANAFUNZI MMOJA AMENASWA AKIUFANYA MTIHANI WA KITAIFA WA KCSE AKIJIFANYA KUWA MTAHINIWA KWA NIABA YA NDUGUYE

Mtihani wa kidato cha nne ksce unaendelea leo hii kwa siku ya tatu baada ya kuanza rasimi jumatatu hii huku waziri wa elimu proff George magoha akiwaagiza wasimamizi wa mitihani kuwa macho ilikukabili udanganyifu
Agizo la magoha limejiri baada ya watahiniwa kadhaa kupatikana na simu pamoja na pesa.
Hiyo jana Polisi kaunti hii ya Pokot magharibi wanamzuilia mshukiwa aliyejifanya kuwa mtahiniwa wa mtihani wa kitaifa kwa kidato cha nne KCSE.
Akithibitisha kisa hicho kamishina wa kaunti hii Apolo Okello amesema kuwa maafisa wa usalama walifuatilia kisa hicho baada ya kupokea fununu ambapo mshukiwa alikamatwa wakati wa mtihani wa kiingereza hiyo jana katika shule ya upili ya mseto ya Werpo Ortum.
Apolo amesema mshukiwa kwa jina Nickson Amani mwanafunzi wa kidato cha tatu katika shule ya upili ya st Anthony Kitale alikamatwa akimfanyia mtihani ndugu yake kwa jina Murunda prince Makawa.
Aidha kulingana na Apolo wawili hao ni wanawe mwalimu mkuu wa shule ya upili ya Werpo Ortum ambapo pia anazuiliwa katika kituo cha polisi cha Chepareria pamoja na wasimamizi wengine watatu wa kituo hicho cha mtihani.
Leo hii watahiniwa wa kcse wanafanya karatasi ya tatu ya kiingereza na karatasi ya tatu ya kemia