WANAFUNZI KUTOKA JAMII MASIKINI WANUFAIKA NA BASARI SABOTI, TRANS NZOIA.

Na Benson Aswani
Zaidi ya wanafunzi 200 kutoka eneo bunge la Saboti Kaunti ya Trans-Nzoia wamefaidi basari kupitia kwa hazina ya fedha za ustawishaji maeneo bunge (NGCDF) chini ya Mbunge Caleb Hamisi.
Akihutubu kwenye hafla ya awamu ya kwanza ya kutoa ufadhili huo kwa wanafunzi, Hamisi amesema hii ni njia moja wapo ya kupiga jeki elimu miongoni mwa wanafunzi kutoka kwa jamii nyingi wasiojiweza eneo bunge hilo.
Aidha Hamisi amesema chini ya miaka minne ya uongozi wake amejenga zaidi ya madarasa mapya 80 ili kuhakikisha miundo msingi bora itakayowezesha utoaji wa elimu bora kwa wanafunzi katika shule za eneo bunge hilo.