WANACHAMA WA CHAMA CHA USHIRIKA CHA METROPOLITAN KAUNTI YA BUNGOMA WATISHIA KUJIONDOA

Walimu wanachama wa chama cha ushirika cha metropolitan katika kaunti ya Bungoma wametishia kujiondoa katika chama hicho kufuatia madai ya kunyanyaswa na kupewa viwango vya chini vya riba licha ya kuwekeza pakubwa katika chama hicho.

Walimu hao wamesema kuwa riba ambayo wamepata mwaka huu ni ya chini sana ambayo ni asilimia tatu ikilinganishwa na asilimia sita ambayo walipata mwaka jana wanayosema iliwawezesha kufanya shughuli zao muhimu.

Walimu hao sasa wanatoa wito kwa vyama vya walimu knut na kuppet kuingilia kati na kuwatetea walimu ambao ni wanachama wa chama hicho cha ushirika huku wakipendekeza kupewa pesa zao ili wawekeze kwingine.

Juhudi za kufikia chama hicho kuhusiana na madai hayo ziliambulia patupu.