WAMILIKI HALALI WA ARDHI TRANS NZOIA WAHAKIKISHIWA USALAMA WA ARDHI ZAO


Serikali imejitolea kikamilifu kusuluhisha mizozo ya ardhi katika kaunti ya Trans nzoia kwa kuwapa hati miliki wamiliki halali.
Kamishina wa kaunti hiyo Sam Ojwang amesema serikali imeendelea kuchapisha zaidi ya hati miliki alfu 12 kuwawezesha wakenya kuwekeza na kuchangia vilivyo ukuaji wa uchumi wa taifa.
Wakati uo huo ojwang amempongeza rais uhuru kenyatta kwa kuzindua mfumo wa kidijitali wa habari kuhusu mashamba kwa jina ardhi sasa ambao amesema utasuluhisha pakubwa mizozo ya ardhi.