WALUKE AAHIDI KUONGEZA IDADI YA WANAFUNZI WANAONUFAIKA NA CDF ENEO BUNGE LA SIRISIA.


Mbunge wa Sirisia kaunti ya Bungoma John Waluke amesema kuwa anapania kuongeza idadi ya wanafunzi watakaonufaika na mgao wa fedha kutoka hazina ya maendeleo ya maeneo bunge CDF eneo bunge hilo.

Akizungumza katika hafla moja ya mazishi eneo la Mwanda wadi ya Malakisi Waluke amesema idadi ndogo ya wanafunzi haswa kutoka divisheni ya Sirisia walisajiliwa kupokea ufadhili wa karo kutoka hazina hiyo huku akiahidi kuongeza idadi zaidi ya wanafunzi.

Wakati uo huo Waluke amesema kuwa wakazi wa Sirisia wamesalia nyuma kimaendeleo kwa muda mrefu kufuatia uongozi mbaya kutoka kwa watangulizi wake, akiwahakikishia wakazi wa eneo hilo kuwa uongozi wake utahakikisha hali hiyo inashughulikiwa.