WALIOPATA DOZI YA KWANZA YA CORONA BUNGOMA WATAKIWA KUJITOKEZA KUPOKEA DOZI YA PILI.


Wakazi katika kaunti ya Bungoma ambao walipokea dozi ya kwanza ya chanjo dhidi ya virusi vya corona wametakiwa kujitokeza na kupokea dozi ya pili.
Waziri wa afya katika kaunti hiyo Anthony Walela amesema kuwa takriban wakazi alfu 34 wamepokea dozi ya kwanza huku alfu sita wakikosa kurejea kupokea ya pili, akiwataka kufanya hivyo ili kupokea kinga dhabiti dhidi ya ugonjwa wa covid 19.
Wakati uo huo Walela amesema kuwa serikali ya kaunti hiyo itahakikisha kila kituo cha afya kinatoa aina moja ya chanjo ili kuzuia visa ambapo wakazi watapokea zaidi ya aina moja ya chanjo akiwataka wakazi kurejea katika kituo walichopokea dozi ya kwanza ya chanjo ili kupokea dozi ya pili.