WALIMU WATAKIWA KUZINGATIA MWONGOZO WA WIZARA YA ELIMU SHULE ZIKITARAJIWA KUFUNGULIWA.


Walimu wakuu katika kaunti ya Trans nzoia wametakiwa kuzingatia mwongozo wa wizara ya elimu sawa na kushauriana na wazazi jinsi ya kulipa karo ya wanafunzi.
Mwakilishi wadi ya Sirende Alfred Weswa amesema biashara za wazazi wengi zilisambaratika kutokana na janga la corona na kuwa si busara kuitisha ada nyingine mbali na karo hasa baada ya muda wa masomo shuleni kupunguzwa kutoka wiki 39 hadi 30 pekee.
Aidha Weswa amewahimiza wazazi kuwatayarisha wanao kwa minajili ya kurejea shuleni wiki ijayo.