WALIMU WATAKIWA KUWA NA SUBIRA KUHUSU MASWALA YA KARO.

Aliyekuwa mshauri wa maswala ya siasa wa gavana wa kaunti hii ya Pokot magharibi Stephen Kolemuk ameshutumu hatua ya kutumwa nyumbani wanafunzi kutafuta karo juma moja tu baada ya kufunguliwa shule nchini.

Kolemuk amesema japo sasa kuna changamoto ya kifedha katika shule nyingi nchini kufuatia janga la corona, walimu wanapasa kuwa na subira na kuzungumza na wazazi kuhusu mswala ya karo na kuwaruhusu wanafunzi kusalia shuleni .

Aidha Kolemuk amesema kuwa hatua ya kutumwa nyumbani wanafunzi kila mara kutafuta karo huenda ikaathiri matokeo ya mitihani ya kitaifa.