WALIMU WATAKIWA KUTOWATUMA NYUMBANI WANAFUNZI KUFUATIA UKOSEFU WA

Mbunge wa kwanza katika kaunti ya Trans nzoia Ferdinand Wanyonyi ametilia mkazo agizo la waziri wa elimu Prof. George Magoha kwa wakuu wa shule nchini kutowatuma nyumbani wanafunzi kwa ajili ya karo.
Wanyonyi amesema kuwa wazazi wanapitia hali ngumu kufuatia kupanda gharama ya maisha hali ambayo imechangiwa pakubwa na ujio wa janga la corona pamoja na kiangazi ambacho kimeathiri pakubwa mapato ya wazazi.
Aidha Wanyonyi amesema kuwa kiwango cha fedha za basari kimeongezwa katika kipindi cha fedha cha mwaka 2022/2023 hali ambayo itawapunguzia wazazi mzigo wa kulipia karo.
Wakati uo huo Wanyonyi ametumia fursa hiyo kutoa wito kwa wakuu wa shule kuwapa wabunge muda wa kulipia fedha za basari kwani kwa sasa bado hawajapokea fedha hizo kutoka hazina kuu ya serikali.