WALIMU WATAKIWA KUTOWAREJESHA NYUMBANI WANAFUNZI SHULE ZINAPOFUNGULIWA LEO.


Shule zinapofunguliwa leo kwa muhula wa kwanza miito imeendwelea kutolewa kwa serikali kuhakikisha kuwa wanafunzi wanasalia shuleni kuhudhuria masomo na kutoruhusu walimu wakuu kuwarejesha nyumbani kutafuta karo.
Wa hivi punde kutoa wito huo ni mbunge wa Kapenguria kaunti hii ya Pokot magharibi Samwel Moroto ambaye amesema kuwa kwa sasa wazazi wengi wanakabiliwa na hali ngumu ya maisha kutokana na athari zilizosababishwa na janga la corona.
Moroto amemtaka rais Uhuru Kenyatta mwenyewe kuangazia swala la elimu na kutomwachia waziri wa elimu prof. George Magoha anayedai ameshindwa kuongoza sekta hiyo kwa kutoa misimamo kinzani kila mara.