WALIMU WAONYWA DHIDI YA KUWAZUIA WANAFUNZI WALIOPACHIKWA MIMBA NA KUJIFUNGUA.
Walimu wakuu katika kaunti hii ya Pokot magharibi wameonywa dhidi ya kuwazuia kurejea shuleni wanafunzi waliopata mimba kipindi walichokuwa nyumbani kufuatia janga la corona na kisha kujifungua.
Spika wa bunge la kaunti hii ya pokot magharibi Catherine Mukenyang amesema kuwa wapo baadhi ya walimu wakuu ambao wamedinda kuwaruhusu wanafunzi hao kurejea shuleni akisema hamna sheria nchini inayomzuia mwanafunzi aliyejifungua kurejelea masomo.
Mukenyang amesema kuwa kujifungua hakuathiri uwezo wa mwanafunzi yeyote kimasomo huku akitoa wito kwa wizara ya elimukaunti hii kuingilia kati kuhakikisha kuwa wanafunzi hao wanafunzi hao wanapata haki yao ya kupata elimu.