WALIMU WAKUMBATIA CBC LICHA YA KUONEKANA KUPINGA AWALI.

Licha ya kuonekana kupinga awali mtaala wa umilisi CBC ulipokuwa ukizinduliwa kwa mara ya kwanza nchini walimu sasa wamekumbatia mtaala huo.
Kulingana na mwalimu mkuu wa shule ya upili ya Asilong kaunti hii ya Pokot magharibi, Richard Kosgei walimu wameukumbatia mtaala huo baada ya kupata mafunzo kuuhusu, huku akiusifia kuwa bora kwa wanafunzi kwani unaleta usawa kwa wanafunzi wote.
Hata hivyo Kosgei amesema kuwa huenda mtaala huo ukawa ghali mno kwa mzazi kutokana na vifaa mbavyo wanahitajika kununua kwa ajili ya matumizi ya wanao kufanikisha masomo yao.
Aidha amesema kuwa wamejiandaa kwa ajili ya wanafunzi watakaojiunga na shule ya upili ya ngazi ya chini yani Junior secondary japo akikiri huenda kukawa na changamoto kwa shule za mabweni hasa baada ya waziri wa elimu Prof. George magoha kusema nyingi za shule hizo zitakuwa za kutwa.