WALIMU NA WANAFUNZI KAUNTI YA POKOT MAGHARIBI WAHAKIKISHIWA USALAMA WAO MSIMU HUU WA MITIHANI YA KITAIFA

Tatizo la usalama ambalo limekuwa likishuhudiwa katika mipaka ya kaunti hii ya Pokot magharibi na kaunti jirani za Baringo, Elgeyo marakwet na Turkana litapata tu suluhu kupitia elimu.
Akizungumza wakati wa kuzindua madarasa yatakayotumika na wanafunzi wa mtaala wa elimu wa CBC katika shule ya upili ya Tapoyo na Murpus kaunti hii ya Pokot magharibi, mkurugenzi wa elimu kanda ya bonde la ufa Jared Obiero amewataka wazazi kuhakikisha kuwa wanao wanahudhuria masomo shuleni.
Obiero amesema kuwa jumla ya madarasa alfu 1,737 yanajengwa eneo la bonde la ufa katika awamu ya kwanza ambapo kufikia sasa madarasa 570 yamekamilika huku wakilenga kukamilisha takriban madarasa 800 kufikia tarehe 7 mwezi huu ambapo mitihani ya kitaifa inatarajiwa kuanza.
Wakati uo huo Obiero amewataka wanafunzi kuwa makini katika kipindi cha majuma saba ambayo watasalia nyumbani baada ya shule kufungwa na kutojihusisha na maswala ambayo huenda yakaathiri masomo yao.