WALIMU CHEPTULEL WAHOFIA USALAMA WAO.


Serikali imetakiwa kuimarisha usalama eneo la Cheptulel mpakani pa kaunti hii ya Pokot magharibi na kaunti jirani ya Elgeyo marakwet iwapo inataka shughuli za masomo kuendelea eneo hilo ambako kulishuhudiwa mauaji ya watu watatu hivi majuzi.
Akizungumza katika kikao maalum kuangazia usalama wa walimu na wanafunzi, naibu katibu mkuu wa chama cha walimu knut tawi la pokot magharibi Raymond Kukotulia ameitaka serikali kuhakikisha kuwa kila shule eneo hilo inalindwa na maafisa wa usalama.
Kwa upande wao walimu wanaofunza katika shule za eneo hilo wakiongozwa na mwalimu mkuu wa sule ya msingi ya Chepkoukou Julius Naera wametaka walimu wa eneo hilo kuajiriwa kufunza katika shule hizo na kuwapa uhamisho walimu kutoka maeneo mengine hadi shule salama.
Ni kauli ambayo imetiliwa mkazo na msimamizi wa wadi ya lomut Nelson Loturiang’iro ambaye amesema kuwa wengi wa walimu hao hawajaripoti shuleni kutokana na hofu ya usalama wao.