WALEMAVU WAFAIDIKA NA MAGURUDUMU KAUNTI YA KAKAMEGA


Mbunge wa kaunti ya Kakamega Bi. Elsie Muhanda anapania kuwasilisha mswada katika bunge la kitaifa wa kutaka viwanda vya humu nchini na sekta mbali mbali kutenga asilimia kumi za ajira kwa watu wanaoishi na ulemavu.
Ameyasema haya wakati wa kupeana vitu vya magurudumu, vyakula na barakoa, kwa watu wanaoishi na ulemavu wadi ya isukha magharibi, eneo bunge la shinyalu akisema nyingi za viwanda vimewatenga wahusika katika nafasi za ajira.
Muhanda ameelezea masikitiko yake kwa kile anachodai idadi kubwa ya walemavu wameondolewa kwenye sajili ya kupokea marupurupu ya kila mwezi kwa njia tatanishi.