WAKUU WA VYUO MAGHARIBI YA NCHI WAITAKA SERIKALI KUTOA FEDHA KWA WAKATI.

Walimu wakuu wanaosimamia vyuo vikuu na vile vya anuwai katika eneo la magharibi ya nchi wameomba serikali kutoa fedha za awamu ya nne kwa wakati unaofaa ili kusaidia matayarisho ya mtihani unaotarajiwa kuanza mwezi ujao.
Wakiongea katika shule ya kitaifa ya kiufundi ya kitale Kaunti ya Trans nzoia baada ya warsha ya siku mbili na maafisa kutoka Baraza la kusimamia mtihani nchini KNEC, wakuu hao walisema gharama ya kutekeleza mtihani huo iko juu na ipo haja ya Serikali kuingilia kati kwa wepesi na kutoa fedha hizo.
Eneo la magharibi lina vyuo hamsini na tano huku mtihani huo ukitarajiwa kwanza mwezi wa Julai.