WAKUU WA USALAMA WALAUMIWA KUTOKANA NA UTOVU WA USALAMA KERIO VALLEY.


Mbunge wa Kapenguria katika kaunti hii ya Pokot magharibi Samwel Moroto amelaumu kile amedai kuwa utepetevu miongoni mwa maafisa wa usalama kufuatia ongezeko la utovu wa usalama katika bonde la kerio.
Moroto amewasuta pakubwa wakuu wa usalama wakiongozwa na waziri wa usalama wa ndani ya nchi Dkt Fred Matiangi na inspekta mkuu wa polisi Hillary Mutiambai anaodai kuwa hawajafanya juhudi za kuhakikisha kuwa visa hivyo vinakabiliwa.
Moroto amesema wawili hao wamedinda kufika eneo zima la bonde la kerio kutathmini hali ilivyo na badala yake kutoa maagizo ambayo hata hivyo hayazai matunda.
Wakati uo huo Moroto ameisuta serikali kwa kufeli kuwahusisha viongozi wa kaunti hii ya Pokot magharibi, Elgeyo Marakwet na Baringo katika kutafuta suluhu ya utovu wa usalama eneo hili hali anayosema imepelekea kuendela kushuhudiwa uvamizi.