WAKUU WA USALAMA KAUNTI YA NAKURU KUWAKABILI WALE AMBAO WANAKIUKA MASHARTI YA KUZUIA MAAMBUKIZI YA CORONA


Wakuu wa usalama kaunti ya Nakuru wameapa kuendeleza msako wa watu wanaokiuka masharti yaliyowekwa na serikali ili kukabili msambao wa virusi vya korona.
Naibu kamishna eneo la Nakuru mashariki Erick Wanyonyi amesema kuwa baadhi ya watu kaunti hiyo wamekua wakikongamana ili kusherehekea au kujiburudisha kwa vileo.
Akiongea baada ya watu 47 kutiwa nguvuni katika kijiji cha Mwariki karibu na Ziwa Nakuru kamanda Wanyonyi amesema kuwa watakaopatikana wakikaidi mwongozo uliowekwa watadhibiwa kisheria.
Aidha wanyonyi amesema kuwa watu wenye vyeo serikalini au jamaa zao na pia mabwenyewe wanaohudumu kwenye kampuni ndio wanaotiwa nguvuni zaidi kwa kukiuka masharti ya kukabili korona.
Washukiwa waliokamatwa wanafikishwa mahakamani asubuhi hii.