WAKUU WA SHULE WATAKIWA KUTOWATUMA WANAFUNZI NYUMBANI.


Miito imeendelea kutolewa kwa wakuu wa shule katika kaunti hii ya pokot magharibi kuwa na subira na kutowatuma nyumbani wanafunzi kutafuta karo.
Wa hivi punde kutoa wito huo ni mwakilishi wadi maalum eneo la Masol Grace Rengei ambaye ameelezea kughadhabishwa na hatua ya baadhi ya shule kuwatuma nyumbani wanafunzi siku chache tu baada ya kurejea shuleni kutoka likizo fupi.
Rengei amesema kuwa kuwatuma nyumbani wanafunzi kutawapotezea muda mwingi ambao wanapasa kuwa darasani wakisoma badala yake akiwahimizalimu kuwasiliana na wazazi kuhusu swala hilo.
Rengei amesema kuwa hatua hiyo ya kuwatuma nyumbani wanafunzi huenda ikatoa mwanya kwa wanafunzi wengi kujihusisha na maswala yanayokwenda kinyume cha maadili kwani wengi wao hawafiki nyumbani kwa wakati.
Ameelezea wasiwasi kuwa kutumwa nyumbani kila mara wanafunzi kwa jili ya karo huenda kukaathiri pakubwa matokeo ya mitihani ya kitaifa kufuatia muda mwingi wanaotumia barabarani huku akiwataka wazazi pia kuwajibikia majukumu yao ya kuwalipia wanao karo.