WAKUU WA SHULE WAONYWA DHIDI YA KUWATUMA NYUMBANI WANAFUNZI.


Baadhi ya viongozi katika kaunti hii ya pokot magharibi wamelalamikia hatua ya baadhi ya shule kuwatuma nyumbani wanafunzi kwa ajili ya karo siku chache tu baada ya wanafunzi kurejea shuleni kutoka likizo fupi.
Aliyekuwa kiongozi wa wengi katika bunge la kaunti hii simon kalekem amewataka walimu kutumia fedha ambazo wizara ya elimu imetuma katika shule pamoja na zile ambazo tayari zimelipwa na wazazi kuendeleza shughuli shuleni na kutowatuma wanafunzi nyumbani kwani kwa sasa wazazi wanapitia hali ngumu kiuchumi.
Aidha kalekem amewataka wakuu wa shule kuwasiliana na wazazi kuhusu jinsi ya kulipa karo ya wanao badala ya kuwatuma wanafunzi nyumbani ambapo wanapoteza muda mwingi barabarani.
Wakati uo huo Kalekem ametoa wito kwa gavana wa kaunti hii John Lonyangapuo kutoa fedha za basari kwa wanafunzi mapema ili kuzuia hali ya wanafunzi kupoteza muda mwingi barabarani wakati huu ambapo uchumi wa wazazi wengi kaunti hii umeathirika pakubwa.