WAKUU WA SHULE WAONYWA DHIDI YA KUWATUMA NYUMBANI WANAFUNZI KIHOLELA.


Wakuu wa shule katika kaunti hii ya Pokot magharibi wametakiwa kuwa na uvumilivu na kutowatuma nyumbani kila mara wanafunzi kutafuta karo.
Ni wito wake mbunge wa Kapenguria Samwel Moroto ambaye amewataka walimu wakuu kuwasiliana na wazazi kuhusu jinsi watakavyolipa karo badala ya kuwatuma wanafunzi nyumbani kila mara huku akisema wazazi wengi kwa sasa wanakabiliwa na hali ngumu kifedha.
Moroto amesema kuwa wataandaa karibuni kikao na wakuu wa elimu katika kaunti hii ya Pokot magharibi li kujadiliana kuhusu jinsi ya kushughulikia swala hili ili kuwapa nafasi wanafunzi kuhudhuria masono ikizingatiwa ufupi wa kuhula huu.
Wakati uo huo Moroto amemsuta waziri wa elimu Prof. George Magoha kwa kile amesema kuwa anatoa maagizo katika sekta ya elimu ambayo hayafuatilii kuhakikisha kuwa yanatekelezwa.